Mahujaji kutoka Iran watashiriki katika ibada ya hijja mwaka 2017 nchini Saudi Arabia.
Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa mahujaji kutoka Iran watashiriki katika ibada ya hijja ya mwaka 2017.
Mahujaji wanaokadiriwa kuwa 85,000 kutoka Iran wanatarajiwa kushiriki katika ibada ya hijja ya mwaka 2017.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mazungumzo kufanyika baina ya Tehran na Riyadh kuhusu usalama wa mahujaji.
Ibada ya Hijja ya mwaka 2017 inatarajiwa kufanyika ifikapo mwezi Septemba.
Mwaka uliopita raia wa Iran hawakushiriki katika ibada ya Hijja kutokana na ajali iliotokea na kupelekea wahujaji wengi kutoka Iran kufariki.
