Kufuata hofu za hujuma za wenye chuki dhidi ya Uislamu, misikiti minne mikubwa nchini Uholanzi itafungwa wakati wa sala baada ya Waislamu sita kuuawa Canada walipokuwa wakiswali msikitini.
Uamuzi huo umechukuliwa na kamati za misikiti nchini Uholanzi, kufuatia hujuma ya kigaidi iliyopelekea Waislamu sita kuuawa na wengine kujeruhiwa walipokuwa wakiswali Sala ya Ishaa katika msikiti mmoja huko Quebec nchini Canada.
Katika taarifa ya pamoja, wasimamizi wa misikiti ya Msikiti wa Samawati mjini Amsterdam, as-Msikiti wa Ahul Sunnah The Hague's, Msikiti wa Essalam mjini Rotterdam na Msikiti wa Omar Al Farouq huko Utrecht wamesema misikiti hiyo wakati wa Sala kwa ajili ya usalama.
Misikiti hiyo huwa na maelefu ya waumini kila siku.
Katika taarifa, Sad Bouharrou, wa Kamati ya Misikiti ya Uholanzi-Morocco amesema, "vitendo visivyo na huruma kama yaliyojiri Quebec huchangua kuenea chuki dhidi ya Waislamu duniani."
Kwa msingi huo baada ya Waislamu kuingia ndani ya msikiti, wakati sala itakapoanza misikiti hiyo itafungwa ili kuzuia hujuma kama ile ya Quebec.
Amesema msikiti huwa wazi wakati wote wa siku kwa ajili ya watu wanaotaka kusali na kupata utulivu lakini amebainisha masikitiko yake kuwa wamelazimika kufunga misikiti wakati wa sala kutokana na kuhofua hujuma za kigaidi.
Uholanzi inajulikana kwa watu wenye chuki dhidi ya Uislamu hasa mwanasiasa Geert Wilders ambaye ni maarufu kwa misimamo yake mikali ya kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu.
Kufuatia ushindi wa Donald Trump mwenye chuki dhidi ya Uislamu katika uchaguzi wa rais Marekani, wanasiasa wenye misimamo mikali ya mrengu wa kulia kote Ulaya nao pia wamepata matumaini ya kunyakua madaraka.
