Tuesday, 31 January 2017

RAIS ADAMA BARROW KUIFANYA GAMBIA KUTOKUWA JAMHURI YA KIISLAMU

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow ameahidi kufanya mageuzi ya sheria kadhaa ikiwa pamoja na kuondoa sheria inayotambua nchi hiyo kama jamhuri ya kiislamu.
Rais Adama aliyazungumza hayo katika mkutano wake wa kwanza tangu achukue Urais wa nchi hiyo.

Rais Adama alisema Alhamis iliyopita kwamba uamuzi huo ulitolewa kwa kuwa wananchi wengi wa Gambia ni waislamu
hivyo ni kuongeza hofu kwa makundi mengine ya dini na ni kinyume na haki za binadamu.
Mnamo Desemba mwaka 2015 rais wa zamani wa nchi hiyo Yahya Jammeh aliitangaza nchi ya Gambia kama jamhuri ya kiislamu. 

Alisema badala ya kuwa Jamhuri ya kiislamu ya Gambia sasa itakuwa jamhuri ya Gambia.