Wednesday, 18 January 2017

MWANAMKE WA KWANZA KULA KIAPO KWA KUTUMIA QURANI BUNGE LA MAREKANI

Ilhan Omar amekuwa mwanamke wa kwanza kula kiapo kwa Qur'ani katika Baraza la Wawakilishi nchini Marekani.
Mnamo Januari 3, Ihan aliapishwa kama mjumbe wa bunge la Baraza la Wawakilishi katika Jimbo la Minnesota na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza Mwislamu Marekani kushika wadhifa huo. 
Ilhan ambaye anawakilisha eneo la House District 60B la Minnesota, ameweka historia kama Msomali-Mmarekani kuchaguliwa kama mbunge nchini Marekani.
ilhan alikula kiapo kwa Qur'ani, na hivyo kuwa mtu wa pili kufanya hivyo baada ya Bw. Keith Ellison kuwa Mwislamu wa kwanza kuchaguliwa katika Bunge la Kitaifa la Congress ya Marekani akiwa Mjumbe wa Jimbo la Minnesota. 

Wawili hao ni wanachama wa chama cha Democratic na Ellison hivi sasa anawania kuwa mwenyekiti Kamati ya Kitaifa ya Chama cha Democratic.

Ilhan Omar mwenye umri wa miaka 34 aliambatana na mumewe aliyekuwa amevaa kanzu, kofia na koti walibeba msahafu mkubwa kwa ajili ya kula kiapo kwa Ilhani.