Chanzo cha ndani ya familia hiyo kinasema mara tu mtoto huyo alipozaliwa alisomewa adhana sikio la upande wa kulia, alirambishwa asali na kuchinjiwa mnyama anayetajwa kuwa kati ya mbuzi au kondoo.
Haqiqa ni sunna anayofanyiwa kila mtoto wa kiislamu anapozaliwa.
Haqiqa ni kuchinja mnyama aina ya Kondoo au mbuzi wawili kwa mtoto wa kiume na mmoja kwa mtoto wa kike.
Mtoto huyo wa kiume ambaye amepewa jina la Eissa Al mana (Issa عيسى) anamfanya Janet kujifungua kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 50.
Maisha ya Janet na mumewe yamekuwa yakiendeshwa kwa usiri mkubwa ili kuepuka waandishi wanaofatilia kila nyendo zao.
Janet aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 50, uvumi wa kuwa mjamzito ulienea kuanzia mwezi April mwaka jana.
Janet anaelezwa kusilimu tangu kuolewa na Tajiri wa Qatar, Wissam Al Mana na mara kwa mara amekuwa akitumia lugha za dini ya kiislamu pamoja na mavazi stara.
