Wednesday, 11 January 2017

MATUKIO YA CHUKI DHIDI YA WAISLAMU YAONGEZEKA AFRIKA KUSINI

Waislamu nchini Afrika Kusini wameelezea hofu yao kuhusu kuongezeka na matukio yanayoashiria chuki dhidi yao.
Siku ya Jumatatu watu wasiojulikana walipaka damu katika kuta za msikiti wa Jamiah uliopo Kalk Bay Capetown, baadaye pia siku ya Jumamosi pua ya nguruwe iliopatikana katika mlango wa msikiti maarufu wa Nurul jijini Cape Town .

Kiongozi wa shirika la mawasiliano la Kiislamu Dk Faisal Suleiman nchini humo alionya serikali kuwa matukio hayo yanayolenga kuwakasirisha waislamu yataendelea kuongezeka ikiwa hatua hazitachukuliwa.

Pia alisema kuwa vyombo vya habari vingine vimechochea matukio hayo dhidi ya waislamu baada ya kuonyesha kuwa waiaslamu ni watu wa ghasia.