Saturday, 7 January 2017

97 WASILIMU KATIKA MSIKITI WA AL-AQSA YERUSALEM

Kwa mujibu wa Imam Sheikh Ekrima Said Sabri  
aliyekuwa Mufti Mkuu wa Yerusalemu takribani watu 100 wamesilimu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Sheikh Ekrima Said Sabri amesema katika ripoti aliyoitoa wiki hii kuwa watu 97 waliosilimu, 17 ni kutoka nchi za magharibi zikiwemo Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Finland.

Watu hao wote wamesilimu katika Msikiti wa Al aqsa ambao ni moja ya Misikiti muhimu katika historia ya uislamu.

Kila mwaka, mamia ya watu kutoka duniani kote hutembelea msikiti wa Al aqsa ulioko Yerusalem ya Mashariki.