Saturday, 3 December 2016

SLOVAKIA YAPITISHA SHERIA YA KUTOTAMBUA UISLAMU KAMA DINI RASMI KATIKA NCHI HIYO

Nchi ya Slovakia imepitisha sheria ambayo itaifanya dini ya kiislamu kutotambuliwa rasmi katika nchi hiyo.
Sheria hiyo iliyopitishwa inaibana dini ya kiislamu kutotambulika rasmi nchini humo ambapo sasa ili kutambulika kwa dini yoyote lazima iwe na wafuasi wapatao 50,000 badala ya 20,000 kama ilivyokuwa awali.

Mabadiliko hayo yanafanya ugumu kwa uislamu kusajiliwa ambapo inaelezwa kuwa na waislamu wapatao 2,000 kwa mujibu wa sensa ya karibuni na hakuna Msikiti unaotambuliwa rasmi.

Taasisi ya Islamic Foundation inatambuwa kuwa na idadi ya waislamu wapatao 5,000 katika nchi hiyo ya Slovakia.

Sheria hiyo ilipitishwa na theluthi mbili ya wabunge wote wa nchi hiyo ambapo wengine walitaka iwekwe idadi ya
wafuasi wa dini wapatao 250,000 ndio itambuliwe kama dini rasmi.
Waziri Mkuu Robert Fico
Slovakia ina idadi ya watu milioni 5.4 na asilimia 62 ni wakatoliki. 

Muswada huu umepitishwa baada ya kupendekezwa na chama cha Slovak National Party (SNS) ambacho kina mlengo wa ukristo katika miongozo yake. 

Mwenyekiti wa chama hicho Andrej Danko alisema
"Ni lazima kufanya kila kitu tunachoweza kufanya kwamba hakuna msikiti utakaojengwa katika siku zijazo."

Kupitishwa kwa sheria hiyo, nae Waziri mkuu wa nchi hiyo alirudia kauli yake kwa kusema uislamu hauna nafasi slovakia.