Saturday, 10 December 2016

AKAMATWA KWA KUHUSIKA NA ULIPUAJI MSIKITI UJERUMANI

Mamlaka nchini Ujerumani imemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusika na kuweka vifaa vya kulipuka katika msikiti mmoja mjini Dresden mnamo mwezi Septemba .
Waendesha mashataka walifahamisha kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 alipatikana na vifaa vya kutengenezea vilipuzi siku ya Alhamis na kukamatwa Ijumaa.

Aidha walisema kuwa ushahidi wa vipimo vyake vya DNA pia vinadhihirisha kuwa ni mmiliki wa vifaa hivyo.

Mnamo Septemba 26 mlipuko ulitokea katika msikiti wa Fatih Camı na kupelekea Imam,mkewe na watoto wawili kujeruhiwa .

Mlipuko huo ulitokea kabla ya kuadhimisha siku ya kitaifa ya Ujerumani mjini Dresden ambapo wengi wa wafuasi wa PEGIDA hupatikana.

Taarifa ya kwanza tuliiandika hapa
Msikiti washambuliwa Ujerumani