Wednesday, 2 November 2016

BAADA YA MIAKA 104 ADHANA KUSIKIKA KATIKA MSIKITI WA HAYDAR KADI, BITOBA NCHINI MACEDONIA

Msikiti wa Haydar Kadı ulioko mjini Bitola kusini magharibi mwa nchi ya Macedonia ambao ni wa utawala wa zamani wa Ottoman unatarajiwa kufunguliwa tena upya hivi karibuni.
Shughuli za ukarabati wa msikiti huo zilianzishwa mwaka 2015 na zimekamilika.

Msikiti wa Haydar Kadı ulijengwa wakati wa utawala wa mfalme Kanuni Sultan Süleyman kati ya mwaka 1561-1562 Macedonia na kufungwa kwa miaka 104.
Msikiti huo kwa miaka kadhaa haukuwa unatumika na badala yake ilikuwa kama sehemu ya maonesho kwa watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Msikiti huo wa kale umekuwa ukistaajabisha wengi kwa namna ulivyojengwa kwa usanifu wa hali ya juu kuanzia minara miwili, mihrabu yake na mapambo kadhaa ya kuvutia licha ya ukongwe wake.
Katika utawala wa Ottoman mji wa Bitola kulikuwa na misikiti ipatayo 70 ambapo kwa sasa imebaki 10 na yenye kusaliwa imebaki minne.