Msikiti mmoja ulioko mjini Orlando katika jimbo la Florida umeripotiwa kushambulia hapo jana nchini Marekani.
Mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa ingawaje hakukuwa na vifo wala majeruhi kutokana na kukosekana watu wakati wa mashambulizi.
Afisa mkuu wa polisi wa mji wa St. Lucie County alitoa maelezo na kuthibtisha kutekelezwa kwa mashambulizi hayo na mshukiwa aliyenaswa na kamera za siri na kuonekana akizunguka nje ya msikiti kabla ya kuuchoma moto nyakati za asubuhi hapo jana siku ya Jumatatu.
Baada ya kuzimwa kwa moto huo, polisi wameanza operesheni ya kumsaka mhusika aliyeonekana kwenye kamera za siri kwa msaada wa wakaazi wa eneo hilo.
Msikiti huo uliokumbwa na mashambulizi unasemekana kutumiwa na Omer Metin ambaye aliwahi kushambulia watu kwa silaha kwenye mgahawa mmoja wa mashoga nchini Marekani.
Omer Metin alisababisha vifo vya watu 49 kwenye mashambulizi hayo na baadaye akaangamizwa wakati wa makabiliano na polisi.
