Saturday, 6 August 2016

BAADA YA MIAKA 150, BUNGE LA UGIRIKI LA PIGA KURA YA NDIO KURUHUSU UJENZI WA MSIKITI KATIKA MJI WA ATHENS

Hatimaye Alhamis Bunge la nchi ya Ugiriki limepiga kura ya kupitisha muswada wa kuruhusu ujenzi wa Msikiti katika mji mkuu wa nchi hiyo Athens.

Zaidi ya kura 200 zilipiga ndio kuruhusu ujenzi wa msikiti, ambapo jumla ya wabunge waliopiga kura ilikuwa ni 230.
Ujenzi wa msikiti katika mji huo uliruhusiwa mwaka 2006 lakini kutokana na misimamo ya kihafidhina, ukiritimba na ya mrengo wa kulia kutoka kanisa la Orthodox na chama cha siasa cha Golden Dawn waliweka zuio la kisheria kutoruhuiwa kujengwa kwa msikiti.

Msikiti huo unatarajiwa kujengwa katika eneo la Elaionas lililo karibu na katikati ya jiji la Athens ambapo zinakadiriwa
Dola milioni moja za kimarekani kutumika kujenga msikiti huo.

Msikiti huo utakuwa na uwezo kubeba waumini 350 chini na juu, sehemu ya maegesho ya magari, sehemu ya michezo na majengo mengine mawili kwa shughuli mbalimbali.

Athens ni moja ya miji mikuu michache ya Ulaya ambayo haina msikiti.

Kwa mara ya mwisho kuwepo msikiti katika mji huo ni pale ulipoanguka utawala Uthmani bin Affan zaidi ya miaka 150 iliyopita. 


Waislamu wanakadiriwa kuwa 300,000 katika mji wa Athens na wamekuwa wakisali katika maghala na sehemu zisizo rasmi kwa ajili ya kutimiza ibada za swala.