Tuesday, 5 July 2016

UTURUKI, NIGERIA ZASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR LEO

Mkurugenzi wa idara ya masuala ya dini nchini Uturuki Mehmet Gormez ametoa ujumbe wa kuwatakia Siku kuu njema ya Eid el Fitri kwa umma wa Uturuki kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan amewatakia waislam siku kuu njema ya eid el Fitri.
Katika ujumbe wake huo kiongozi huyo amewatolea waislamu wito wa kuchangia furaha ya siku kuu hiyo kama alivyo fundisha Mtume.

Ujumbe huo ulitolewa Jumatatu kuamkia Jumanne ambapo waislamu nchini Uturuki wanasherehekea kumalizka kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Nchi zingine iliyosherehekea sikukuu ya Eid el Fitri ni Nigeria(Baadhi wamefunga), Afghanistan, Indonesia, Bosnia, Kyrgyzstan, Uholanzi, Russia, Australia na Macedonia.

Wakati huo huo, Kiongozi wa baraza kuu la waislamu nchini Nigeria (NSCIA) Sheikh Alhaj Sa'ad Abubakar amesema kuwa hakuna sehemu yoyote ya nchi hiyo ulipoonekana mwezi, hivyo kuwataka waislamu wa nchi hiyo kuendelea na funga ya Ramadhani.

Sheikh Alhaj Sa'ad Abubakar amesema sikukuu ya Eid El Fitr inatarajiwa kuwa siku ya Jumatano. Hata hivyo sehemu kadhaa za nchi hiyo wamesherehekea sikukuu ya Eid El Fitr leo.