Askari wa Marekani anaetambulika kwa jina la Petrie ambae ni rubani katika kambi ya İncirlik amesilimu na kuwa muislamu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Saudi Arabia ni kwamba rubani huyo alitoa shahada katika mskiti Incirlik na kukiri kuwa muislamu.
Video moja ilionesha rubani huyo kutoka Marekani akiwa pamoja na wanajeshi wa Saudi Arabia alitoa shahada katika mskiti huo Incirlik.
Video hiyo imeonekana kwa kiasi kikubwa katika mitandao ya kijamii.
