Tuesday, 17 May 2016

MTANZANIA ASHIKA NAFASI YA SITA MASHINDANO YA USOMAJI QURANI DUNIANI

Msomaji Qurani (Tajweed) wa Tanzania Ustaadh Rajai Ayoub ameshika nafasi ya Sita katika Duru ya 33 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani yaliyofanyika mjini Tehran nchini Iran.

Mashindano hayo yalianza rasmi siku ya Jumatano katika Ukumbi Mkubwa wa Swala wa Imam Khomeini MA na yamemalizika leo Mei 17.
Rajai akiwa na zawadi yake
Katika Mashindano hayo Msomaji wa Iran Hamed Valizadeh ametangazwa kuwa mshindi wa kwanza. 

Rajai Ayoub alifanikiwa kupita katika mchujo wa washiriki 57 waliochuana kutoka nchi mbalimbali duniani na kuwa miongoni wa sita bora waliopambana kumpata mshindi wa kwanza.
Washiriki
Mohammad Javid Akbari kutoka Afghanistan ameshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Bahre Al Din Saeed kutoka Indonesia.

Nafasi ya nne ilichukuliwa na Syed Abbas Ali kutoka nchi ya Ujerumani na nafasi ya tano ilichukuliwa na Mustafa Ali kutoka Uholanzi.
Palipofanyikia mashindano
Nafasi ya sita ilichukuliwa na Mtanzania Rajai Ayoub.
Aidha katika upande wa kuhifadhi nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Mojtaba Fard Fani ambaye nae ni raia wa Iran.

Nafasi ya pili na ya tatu ilichukuliwa na Abdul Aziz Ahmed kutoka Misri na Muhammad Ali Abdullah kutoka Australia.
Nafasi ya nne ilichukuliwa na Khalid Sankari from kutoka Ivory Coast na Muhammad Taha Hassan kutoka Niger.

Nchi 70 zilituma wawakilishi wao katika mashindano hayo ambayo kauli mbiu yake ni 'Kitabu Kimoja Umma Moja'..