Tuesday, 24 May 2016

"HESHIMUNI HIJABU KWA WANAWAKE WA KIISLAMU" PAPA AIAMBIA UFARANSA

Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amewataka wafaransa kuheshimu haki za wanawake wa kiislamu na kuitambua imani yao kwa kuvaa Hijabu kama vile wanavyotambua kwa wakristo kuvaa msalaba.

"Kama wanawake wa kiislamu wanapenda kuvaa Hijabu basi lazima wawe na uwezo wa kufanya hivyo, na vile vile kama wakatoliki wanapenda kuvaa msalaba. Watu lazima wawe huru katika kuitekeleza imani yao katika mioyo yao kwa uwazi na wala siokatika maeneo ya kujificha", alisema Papa Francis kuliambia Gazeti la kikatoliki la Ufaransa la La Croix.
Ufaransa inakadiriwa kuwa na waislamu Milioni sita na kuwa nchi yenye waislamu wengi zaidi barani Ulaya.

Kwa muda mrefu waislamu wamekuwa wakilalamika vikwazo vya kutekeleza imani yao kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.

Mwaka 2004 Ufaransa ilipiga marufuku uvaaji wa Hijabu katika ofisi za umma na katika shule. Mwaka 2011 pia ilipiga marufuku uvaaji wa Niqabu.