Leo ni tarehe 1 ya mwezi wa April ni siku ambayo 'huitwa' ni 'April Fool' yaani siku ya wajinga duniani.
Siku hii hutumika kwa watu wengi kufanya matukio ya uongo kwa wenzao. Au namna mbalimbali za hadaa ili tu kuwashungulisha, kuwaudhi ama kuwatisha na mambo kadhaa ya kipuuzi.
Bahati mbaya washiriki wa ujinga huo wapo baadhi ya waislamu. Hushiriki ujinga huo ama kwa kutojua au kwa kujua.
Hapo chini kuna maelezo ya Mtume wetu Muhammadﷺ akitahadharisha waislamu na uongo.
Mtume Muhammadﷺ anasema:
"Uongo ni haramu japokuwa ni maskhara"
Katika jambo la kusema uongo waislamu wamekatazwa na wametakiwa kuwa nalo mbali kabisa na kuna maonyo makali kutoka kwa mtumeﷺ pale aliposema:
"Ole wake kwa anayehadithia jambo la uongo ili watu wacheke. Basi ole wake! Ole wake".(Tirmidhiy na Abu Daud)
Pia mtumeﷺ anasema: "Hakika mimi nafanya mzaha lakini sisemi ila tu yaliyo ya kweli".(At twabaraniiy)
Pia tusisahau kauli ya mtumeﷺ pale aliposema:
"Alama za munafiq ni tatu; akizungumza husema uongo, akitoa ahadi haitimizi, akiaminishwa kwa kitu hufanya hiyana"
(Bukhaary na Muslim)
Allah atujaalie tuwe wale wenye kuambiwa mazuri na kuyafanyia kazi na tukikatazwa mabaya kuyaacha.
