Monday, 4 April 2016

MSIKITI, KITUO CHA UTAMADUNI WA KIISLAMU VYAZINDULIWA MARYLAND NCHINI MAREKANI

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezindua kituo cha utamaduni wa kiislamu Lanham, jimbo la Maryland karibu na Washington D.C katika ziara yake nchini Marekani.

Katika uzinduzi huo rais Erdogan alifahamisha kuwa kituo hicho ni kwa niaba waislamu wazuri wenye moyo na imani yao na kuonesha falsafa za kiislamu.
Msikiti huo umezinduliwa katika wakati ambao waislamu kwa ujumla wamekuwa wakitendewa matendo yasiyo ridhisha na watu wasioutambuwa uislamu na mafunzo yake.

Ugaidi, ubaguzi, na maovu mengine ni matendo ambayo yanapingwa vikali na mafunzo ya uislamu alibainisha rais Erdogan.

Aidha baada ya kufungua msikiti huo Rais Erdogan alisoma Qurani kwa njia ya Tajweed.