Sheikh wa taasisi ya kidini ya Al azhari shariif imamu mkuu Dr Ahmad Twayyib ametoa wito wa kuboreshwa majadiliano ya ulimwengu kwa lengo la kusimamisha vita na umwagikaji wa damu pamoja na kupambana na tatizo la ugaidi, kisha fedha zinazotumika katika vita zielekezwe kwa mafakiri.
Hayo yamekuja kufuatia makutano aliyofanya Dr Ahmad Twayyib mwanzoni mwa wiki pamoja na ujumbe wa wamarekani uliowajumuisha wanasiasa,viongozi wa dini ya kikristo na wawakilishi wa taasisi za kiraia,ujumbe ambao upo ziarani jijini Cairo.
Kwa upande wake ujumbe huo ulitoa pongezi zake kwa Al azhari shariif na nafasi yake katika kupambana na siasa kali huku wakisisitiza upingaji wao wa wazi matamshi ambayo yamekuwa yakitumiwa na baadhi ya watia nia katika kampeni za uraisi nchini Marekani,na kuongeza ya kuwa kauli hizo zasababisha chuki baina ya raia.
