Wednesday, 16 December 2015

KUMBUKUMBU: MUHAMMAD ALI AKIWA NA WANAFUNZI WA MADRASA AKISOMA DUA

Mwaka 1988 Novemba 23, Muhammad Ali alitembelea nchi ya Sudani na moja ya fursa aliyopata ni kutembelea vijana wa Madrasa wa Msikiti wa Dafaalah el Sa'em ulioko Khartoum.

Mbali na kuongea nao pia alifanya dua ambayo mpaka leo ipo katika kumbukumbu ya watu wa eneo hilo.
Akifanya Dua
Muhammad Ali  alizaliwa mnamo 17 Januari 1942 ni mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. 

Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Huyu anatazamika kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote. 

Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olompiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini Rome, Italia.

Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, amekwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. 

Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la 'Mwanamichezo wa Karne' na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.

Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni 'napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki'.

Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964, baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975. 

Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. 

Alikamatwa na kupatikana na mashtaka, na wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. 

Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.

Muhammad ali ana watoto ana watoto tisa ambao ni Laila Ali, Rasheda Ali, Asaad Amin, Hana Ali, Jamillah Ali, Khaliah Ali, Muhammad Ali Jr., Maryum Ali, Miya Ali