Navi Pillay amesema watoto katika taifa hilo wamekuwa wakikatwa katwa vipande na wauaji wamekuwa wakila nyama ya watu wanao wauwa.
Aliongeza kusema kuwa chuki baina ya jamii zimefikia kiwango cha kutisha, na kwamba watu wamekua wakiteswa na kuchomwa .
Hata hivyo amesema kupelekwa huko kwa vikosi vya Ufaransa na Afrika kumepunguza kiwango kikubwa cha mauaji kwa sasa.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika dimbwi la ghasia baada ya waasi kuchukua mamlaka mwezi Machi mwaka jana.
![]() |
| Navi Pillay |
