Friday, 21 March 2014

MSIKITI WAHARIBIWA, QURANI TUKUFU YACHANWA NA KUCHOMWA MOTO ROMA, ITALIA

Msikiti wa Amani (Mosque of Peace) uliopo kilomita 80 kutoka mji wa Roma jumapili usiku ulivamiwa na watu wasiojulikana na kuharibiwa ikiwemo kuchanwa na kuchomwa moto Qurani Tukufu.

Msikiti wa Amani (Mosque of Peace) upo katika mji wa Rieti, mkoa wa Lazio

Gazeti la Italia la Ilmessaggero liliripoti kuwa watu hao wasiojulikana walichoma Qurani, waliiba Fedha, waliharibu maandishi yaliyokuwa ndani ya msikiti na kuharibu sehemu ya Mihrabu ya msikiti huo. 

Viongozi wa kiislamu kupitia jumuiya ya 'Salsabil' wameshutumu kitendo hicho cha uharibifu wa mali za msikiti kwa kusema hiyo ni dalili mbaya ya mahusiano na kutovumiliana katika tofauti za dini.

Aidha, Viongozi wa italia wameonesha mshikamano na jamii ya kiislamu baada ya kutoa tamko kali la kulaani kitendo cha watu wasiojulikana kuvamia msikiti wa Amani (Mosque of Peace) katika mji wa Rieti katika mkoa wa Lazio na kuharibu mali za msikiti  ikiwemo kuchana Qurani Tukufu.

Meya wa mji wa Rieti Simone Petrangeli alionesha mshikamano kwa jamii ya kiislamu kwa kukemea na kuwalaani wote waliohusika na uharibifu wa msikiti huo. 

"Hawa ni watu wabaya ambao wanataka kudhoofisha amani na kuvumiliana katika mji. Wanataka kudhoofisha mshikamano kati ya jamii tofauti katika wilaya ya Rieti", alisema kwa hasira.

Nchi ya italia ina idadi ya waislamu milioni 1.7.


Qurani ikiwa imechomwa moto
Qurani Tukufu ikiwa imechanwa Msikiti wa Amani huko Italia