Kaimu Hakimu Mkuu wa Nairobi Daniel Ochenja alitoa uamuzi huo kuwa ni kwa maslahi ya umma kuwa washukiwa hao wabakie chini ya ulinzi, hasa kutokana na ukubwa wa kesi, ambayo hubeba adhabu ya kifo, na uwezekano wa washukiwa kutoroka.
Alikataa hoja ya wakili wa washukiwa hao Mbugua Mureithi, ambaye alisema kwamba washukiwa walikuwa tayari na nia ya kutimiza matakwa yoyote ya dhamana.
"Kwa sababu za kiusalama, naona haifai kuwaachia watuhumiwa hao kwa dhamana," Ochenja aliamua. "Usalama wao uko katika ulinzi", aliongeza.
Watu wanne hao, Adan Mohamed Abidkadir Adan, Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah Omar na Hussein Hassan Mustafa, watabakia kizuizini katika muda wote wa kesi zao. Wote walikana mashtaka hayo.
![]() |
jengo la westgate kabla ya kuvamiwa |