kwa kudhalilishwa, kupigwa na kulazimishwa kuondolewa katika jengo hilo kwa sababu ya kufanya ibada ya swala ndani ya jengo hilo.
Kwa mujibu gazeti la New York Post wanandoa hao wanamshitaki mmiliki wa jengo hilo lilipo katika jiji la New York, Marekani pamoja na kampuni ya ulinzi ya Andrews International Inc kwa tukio hilo lililotokea julai 2 mwaka 2013 katika ghorofa ya 86 ya jengo hilo.
Wanandoa hao waliokuwa na watoto wawili walipanda jengo hilo refu (skyscraper) kama sehemu ya utalii na ulipofika muda wa swala ya Magharibi waliamua kwenda eneo lenye utulivu na kuanza kusali.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Post walipoanza kusali walifika walinzi wawili na kuanza kuwapiga mateke na kisha kuwatoa katika jengo hilo.
Wakili wa wanandoa hao Phil Hines alisema kuliambia gazeti la New York Post kwamba Jengo la Empire State limekuwa ni 'Ujenzi wa ujinga na Dhulma'.
Alisema safari ya furaha ya familia hiyo ilikatwa muda mfupi tu baada ya maafisa wa usalama kuwatoa nje ya jengo hilo kwa sababu ya kuamua kutekeleza imani ya dini yao.
Wakili Phil Hines alisema wamefungua kesi ya madai ya kutaka kulipwa Dola milioni tano kama fidia ya kudhalilishwa na kupigwa kwa wateja wake.
| Skyscraper |