Monday, 24 March 2014

MAANDAMANO MAKUBWA YAFANYIKA GAZA KUMKUMBUKA SHEIKH YASSIN

Maelfu ya wapalestina jana jumapili wamejitokeza Gaza kukumbuka kifo cha Sheikh Ahmed Ismail Yassin Hassan الشيخ أحمد إسماعيل حسن ياسين‎ aliyeuawa na Wayahudi 22 Machi 2004 pamoja na watu wengine 10.

Sheikh Ahmad Yassin alikuwa ni mwanachuoni na kiongozi wa kiroho wa Harakati za Mapambano ya Kiislamu ya Palestina katika chama cha Hamas.

Sheikh Ahmad Yassin aliuawa mara baada ya kumaliza kuswali Sala ya Alfajiri katika Msikiti mmoja ulioko eneo la Ukanda wa Gaza, baada ya kushambuliwa na helkopta za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ismail Haniyeh, mkuu wa serikali ya Hamas aliuambia umati wa watu uliojitokeza kwamba mauaji kwa watu Gaza yakome kwani kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiishi kwa hali za wasiwasi.

Alisema watu wa Gaza wamekuwa wakipita katika kipindi kigumu na changamoto kali kwa hiyo jihad kwa watu wa Gaza si dhambi kwa namna wanavyouawa bila sababu.

Mkutano huo wa hadhara ulikuwa na lengo la kuadhimisha viongozi wa juu wa Hamas ikiwemo na mwanzilishi wa kundi hilo Sheikh Ahmed Yassin.


Maelfu ya waandamanaji
Kijana wa Kipalestina
Ismail Haniyeh