Saturday, 22 March 2014

BUNGE LA KENYA LAPITISHA MUSWADA WA RUHUSA YA MWANAUME KUOA WANAWAKE WENGI

Bunge la Kenya Alhamisi lilipitisha sheria ya ruhusa kwa wanaume kuoa wanawake wengi watakavyo bila kuwa na ridhaa ya mke wa kwanza, Gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.

Wanasheria walipiga kura kuondoa kifungu katika Mswada wa Sheria ya Ndoa kinachomtaka mume katika ndoa ya kimila kumweleza mkewe kabla ya kuoa mwanamke mwingine. Baadhi ya wanawake wanawake walionesha kuchukizwa kwao na marekebisho hayo kwa kutoka nje ya bunge.

Mswada huo pia ulitoa uamuzi kwamba ndoa zote zinapaswa kusajiliwa na kuweka kiwango cha chini cha umri wa ndoa, kuzuia watoto, hususan wasichana, dhidi ya kuolewa mapema.

Hata hivyo, kiongozi wa wengi Aden Duale, alichukulia suala hilo pamoja na kifungu cha usajili, akisema kitaathiri ndoa za Kiislamu ambazo hazihitaji usajili.

"Katika jimbo lililopanuka ninaloishi, watu wawili wanaweza kuamua kuoana msikitini na wanachukuliwa kama ndoa, Kutosajili hakutengui ndoa", aliongeza.

Katika dini ya Uislamu mwanaume amepewa ruhusa ya kuoa wanawake wanne tu.


Bunge la Kenya