Wakimbizi 1,000 Waafrika wameandamana katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu wakilaani sera kibaguzi za utawala wa Israel.
Maandamano hayo yamefanyika mkabala ya jela la wazi katika eneo la Holot siku ya Jumatatu.
Waandamanaji hao wametaka watu wote wanaoshikiliwa katika kizuizi hicho cha kuogofya kuachiliwa huru na kutambuliwa kama wakimbizi.
Makumi ya maelfu ya wahamiaji kutoka nchi za Kiafrika zinazokumbwa na migogoro kama Eritrea na Sudan wamekimbilia Israel.
Hata hivyo hawajapata afueni kama walivyotarajia bali hali zao ni mbaya zaidi kuliko mapigano waliyoyakimbia kwani wanakumbana na sera rasmi za ubaguzi wa rangi katika utawala wa Kizayuni.
Katika wiki za hivi karibuni maelfu ya wahajiri wa Kiafrika wamekuwa wakiandamana katika barabara za Tel Aviv wakipinga siasa za utawala huo ghasibu kuhusiana na wahajiri.
Hivi karibuni ilibainika kuwa wahajiri wa Kiafrika huko Israel wanatumika kama panya wa maabara na vile vile viungo vyao muhimu vya mwili kama figo huondolewa na kuuzwa bila idhini yao.
