Ofisi ya Kurugenzi Kuu ya msikiti Mtakatifu wa Makkah, ambao una lengo la kutoa huduma bora kwa mahujaji watakaokwenda Hajj na Umrah.
Katika kufanikisha hilo Ofisi ya Kurugenzi, imeamua kushirikiana na Chuo Kikuu cha Umm Al-Qura cha Mecca, Saudi Arabia. Mafunzo ya kozi hiyo ni hatua ya kwanza kwa ushirikiano baina ya Kurugenzi na chuo hicho.
Lengo kuu ya kozi hiyo ni kuwaelimisha wafanyakazi wanaohudumia mahujaji ili kuleta ufanisi katika huduma wazitoazo. Aidha washiriki pia watapewa mafunzo ya lugha za Kiingereza, Urdu, Kiajemi na Kifaransa kwa ajili ya kuwasaidia kuwasiliana na mahujaji.
Mahujaji na wafanyakazi wakati mwingine huwa na matatizo kutokana na ukosefu wa kutokuelewana katika lugha za mawasiliano.
![]() |
| Masjid al haram |
