Mahakama ya Kenya Jumatatu (tarehe 3 Februari) iliwashtaki vijana 129 kwa kuwa wanachama wa Al-Shabaab kufuatia uvamizi wa polisi kwenye msikiti wa Masjid Mussa wa Mombasa Jumapili.
Wanne kati ya washukiwa wanashikiliwa chini ya ulinzi wenye silaha katika hospitali kuu ya Pwani wakati wakipata matibabu ya majeraha waliyoyapata wakati wa makabiliano katika Masjid Mussa.
Baraza Kuu la Waislamu la Kenya (SUPKEM) lililaani vijana waliokamatwa na matumizi ya msikiti kwa shughuli za uhalifu, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti.
"Baraza Kuu la Waislamu la Kenya limeshtushwa na tamko la shughuli za kinyume na sheria, uhalifu na vitendo visivyo vya Kiislamu vilivyofanywa na vijana wanaofanya ujambazi katika msikiti wa Mussa huko Mombasa," Katibu Mkuu wa SUPKEM Adan Wachu alisema katika taarifa.
"Hatuwezi kusema aina ya imani walioiwakilisha na kuhusiana na hilo, tunawakana kabisa hao"
"Kile ambacho vijana wanadai kufuata Uislamu wanachofanya hakipo kwenye Qurani wala kwenye maneno ya mtume," alisema, alisema na kuongeza kuwa, "Tunatoa wito kwa Waislamu wote kuungana dhidi ya mnyama huyu. Uislamu siyo ugaidi, wala ugaidi si Uislamu."
Kamishina wa Kaunti ya Mombasa Nelson Marwa alitahadharisha kwamba kuna hatari ya kufungwa kwa msikiti wa Masjid Mussa kama viongozi wa eneo hilo watashindwa kutatua matatizo yanayoathiri msikiti huo.
