Rais Museveni amesema haelewi ni kwa nini mashoga wahavutiwi na ‘wanawake hawa warembo’ na badala yake kuvutiwa na wanaume wenzao.
"Hadi sasa sijaelewa kikamilifu ni kwa nini unaweza kukosa kuvutiwa na wanawake hawa warembo na uvutiwe na mwanaume mwingine. Hili ni tatizo kubwa,” alisema.
Museveni pia ameshambulia mataifa ya nje ambayo yamekuwa yakimtaka asitie saini mswada huo pamoja na viongozi wa kidini.
“Watu kutoka nje hawawezi kutuamuru tufanye au tusifanye mambo. Kama hawataki kwenda nasi, basi wanaweza kuchukua misaada yao," alisema katika ikulu ya Entebbe.
“Kumbuka Yesu aliuawa na Maaskofu, ndio maana huwa sisikizi hawa watu (viongozi wa kidini)”, alisema.
![]() |
| Yoweri Museveni |
