Monday, 10 February 2014

MAHUBIRI YA DR. ZAKIR NAIK YASILIMISHA WATU 10 RIYADH

Wanaume sita na wanawake wanne wamesilimu kufuatia mahubiri (Da'awa) ya Dr Zakir Abdul karim Naik aliyoyatoa katika ukumbi wa king Fahd Cultural Center huko mjini Riyadh,Saudi Arabia.

Akiwahutubia wasiokuwa waislamu aliwaambia kwamba, "Uamuzi bora wa maisha yako ni kuchagua dini ya haki. Kuukubali Uislamu kama njia ya maisha ni rahisi sana. 
Ni kutamka Shahada kutangaza kwa kusema la ilaha illallah muhammad ar rasulullah لا إله إلا الله محمد رسول الله (Hakuna mungu apase kuabudiwa ila Mwenyezi Mungu na Muhammad ni mjumbe wake).

Catherine Villahermosa , kutoka Philippines ambaye amekuwa akiishi Saudi Arabia tangu 2010 , alisema, "mwajiri wangu aliwahi kunipa nakala ya Qur'an katika lugha yangu ya asili baada ya kutambua maslahi yangu katika Uislamu. 

Nilianza kusoma pole pole na kuanza kuelewa ufunuo wa 

Mungu. Na nilipomsikiliza zakir Naik kusikiliza na wito wa moyo wangu na niliamua kusilimu.

Hanadi Mohammed ambaye ni mwajiri Villahermosa alisema, "Nilisubiri hapa siku nzima kwa ajili ya Catherine katika kubadilisha maisha yake. Nina furaha sana kwa ajili yake".

Wengine waliosilimu ni Jeneline Mimita, Giovannie Bouzan ambaye ni nesi katika Hospitali ya King Fahd na Nabe Muhi kutoka nchi ya Philippines.

Dr. zakir,48 mwenye asili ya India na uraia wa Uingereza amekuwa akizunguka katika nchi mbalimbali duniani na kufanya mihadhara inayojenga imani kwa waislamu na kuwavutia wasio waislamu kuingia katika uislamu.


Dr. Zikir Naik
Catherine Villahermosa (Kulia) na Nabe Muhi (Kushoto) ambao
 wamesilimu kutokana na Da'awa Zakir Naik