Fatou Bensouda Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC amesema kuwa, hali ni ya kusikitisha nchini humo, na kusisitiza kwamba washukiwa wote wanapaswa kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka.
Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, hivi karibuni kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti Balaka limekuwa likifanya jinai, ukandamizaji na mauaji dhidi ya Waislamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Karibuni, Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu limetaka vyombo vya sheria vya Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchunguzi na kubaini jinai zilizotendwa na makundi mbalimbali nchini humo kama vile wanamgambo wa Seleka, Anti Balaka na hata vikosi vya jeshi la serikali ya nchi hiyo.
Imeelezwa kuwa, zaidi ya watu 1,000 wameuawa tokea kundi la Anti Balaka lianze kufanya mauaji dhidi ya Waislamu wiki chache zilizopita.
![]() |
| Fatou Bensouda |
