Kundi la askari wapatao 20 wa Jamhuri ya Afrika ya kati wamempiga na kumuua muislamu waliyemdhania ni Askari wa kundi Seleka dakika chache baada ya kusikia rais mpya wa mpito wa nchi hiyo Catherine Samba - Panza kutaka kutangaza kurejesha amani kwa kuligawa jeshi la nchi hiyo.
Shirika la habari Reuters limesema liliwaona askari wapatao 20 waliovalia sare za kijeshi wakimchoma choma kwa visu mtu huyo mpaka kumuua.
Tukio hilo lilifanyika kabla ya dakika kumi Rais kuwahutubia wanajeshi wapatao 1,000 ambapo ni umbali wa mita 20 toka sehemu ambayo alitarajiwa kuhutubia.
Watu milioni moja wameyakimbia makazi yao na watu wapata 2,000 wameuawa tangu kuanza kwa mapigano nchini humo.
Waislamu nchini Afrika ya kati ni asilimia 15 ambapo wamekuwa wakipigwa na kuuawa kila kukicha.
Angalia picha za muislamu huyo namna alivyouawa na kisha maiti yake kuburuzwa mitaani huku ikidhalilishwa na kupigwambele ya kadamnasi ya watu.
'Eeeh!! Mateso kwa waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati'

















