Msemaji wa utawala wa Benadir Mohamed Yusuf Osman aliiambia Sabahi News kwamba mlipuko huo uliwaua askari watatu na raia tisa, na kujeruhi wengine sita.
Shambulio hilo la ulipuaji mabomu la Al-Shabaab ndani na kuzunguka Mogadishu ni dhahiri kwamba limetokea miongoni na ghafla. Umetokea katika kipindi cha chini ya wiki baada ya wanamgambo hao kutekeleza shambulio la kujitoa muhanga lililosababisha vifo huko Villa Somalia.
"Tumetekeleza ulipuaji bomu dhidi ya maofisa wa usalama wa taifa", msemaji wa Al-Shabaab Abdiaziz Abu Musab aliiambia AFP, akijigamba kuua watu 11, wakiwemo maofisa waandamizi.
Baadhi ya mashuhuda walidokeza kwamba mlipuko huo ulifanywa na mlipuaji wa kujitoa muhanga aliyekuwa akiendesha gari, ambaye walisema aligeuka ghafla kuingia kwenye mgahawa karibu na ufukwe wa Lido.
Askari walifyatua risasi hewani baada ya mlipuko huo ili kufanya mkusanyiko wa watu urudi nyuma, kwani baadhi ya raia walikimbilia kuwachukua waliojeruhiwa kwa kutumia mashuka kama machela ya muda. Baadaye magari ya kubeba wagonjwa yaliwasili kuwachukua waliojeruhiwa.
Abdi Mohamud, meneja wa mgahawa wa Suubiye, aliiambia Sabahi News kuwa alikuwa njiani kurejea kutoka chuoni kwenye masomo ya asubuhi wakati shambulio hilo lililopotokea na aliwasili kwenye eneo la tukio hilo dakika chache baada ya mlipuko huo.
"Mgahawa wetu unatoa huduma ya chai na vitafunwa laini, hutembelewa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo baadhi ya waajiriwa wa serikali, lakini sijui ni kwa nini tulikuwa tunalengwa," alisema.
Mohamud, ambaye familia yake inamiliki mgahawa huo, alisema kwamba inatia wasiwasi kwamba eneo hilo kwa kuwa karibu na Shirika la Upelelezi la Taifa siyo salama.
Dahir Ali, dereva teksi ambaye alikuwa amesimamisha gari barabarani hapo kutoka kwenye mgahawa huo wakati wa mlipuko, alisema aliingiwa na hofu kubwa.
"Ulikuwa mlipuko wa ghafla. Niliona moshi mweusi na singeweza kutafuta suluhisho [sababu] kwa wakti huo huo," aliiambia Sabahi.
Sekunde chache baada ya mlipuko huo, huku moshi ilipokuwa ikiisha, alisema aliona sehemu za miili ya watu zikiwa zimekatika vipande vipande ambao walikuwa kwenye mgahawa huo na gari lililokuwa likichomeka.
"Mungu atuepushe na al-Shabaab," alisema ."Ukizingatia kwamba wanaua watu, siwezi kusema kwamba al-Shabaab wanahusiana na Uislamu kwa chochote."
Muna Ahmed, mwenye umri wa umri wa miaka 36 mama wa watoto sita ambaye anaishi karibu na mgahawa huo, alisema alikuwa anaomboleza kwani alikuwa anawajua baadhi ya wafanyakazi kwenye mgahawa huo ambao walifariki dunia. Baadhi ya wakina mama waliouawa walikuwa wajane wenye watoto na ndio walikuwa watafutaji pekeke wa riziki kwa kaya zao, alisema
"Wakati tuliposikia mlipuko huo tulijifungia [majumbani] na watoto wetu," aliiambia Sabahi News. "Watoto wetu walijua papo hapo kwamba nani walihusika na mlipuko huo, ni ukweli unaojulikana kwamba Al-Shabaab inalenga raia."
Waziri mkuu wa Somalia Abdiweli Sheikh Ahmed alikariri mipango ya serikali yake kuimarisha usalama katika mji mkuu na kuiondoa kabisa al-Shabaab.
"Shambulio la leo la kutobagua katika mgahawa wa chai uliojaa watu wanaoendelea na maisha yao umesababisha upotevu mkubwa wa Wasomali wasiokuwa na hatia," alisema katika waraka wake". Ajenda ya Al- Shabaab ni uasi wa Uislamu na Jamii za Somali zenye amani wanaopenda kuona watu wapya, utulivu na Somali iliyoungana."
![]() |
| Viongozi wa Al-Shabab |
