Mwanamke wa kiislamu amelipwa kiwango cha dola 85,000 nchini Marekani kwa kuwa alikamatwa na kulazimishwa kuvua hijabu rumande Long Beach Los Angeles, California.
Mwanamke huyo ambae alifahamika kwa jina la Kirsty Powell aliwafungulia mashtaka askari wa kiume waliomkamata na kumlazimisha kuvua hijabu kipindi alipokuwa rumande.
Mwanamke huyo alilala rumande kwa usiku mmoja ambapo alilazimishwa kutokuwa na hijabu katika usiku huo ambapo ni kinyume na utaratibu wa dini yake.
Mumewe Powel aliwaomba askari wa kike ndio wahusike katika shauri lake lakini maafisa wa Polisi walikataa ombi hilo.
Kirsty Powel alikamatwa na Askari mwaka 2015 akiwa na mumewe wakiendesha gari ambapo ndipo mzozo huo ulipoanzia.
Mwanamke huyo alifungua mashtaka kwa kuwa alilazimishwa kuvua hijabu mbele ya askari wa kiume na watu wengine waliokuwa wamekamatwa.