Thursday, 20 July 2017

JAJI AMZUIA MWANAMKE KUINGIA MAHAKAMANI KWA SABABU YA HIJABU

Jaji mmoja nchini Ujerumani amempiga marufuku Najat Abokal, mwanamke wa kiislamu mwenye asili ya Syria kuingia katika mahakama akiwa amevaa Hijabu.
Mwanasheria wa mwanamke huyo alisema amri hiyo ilitolewa wakati wa kusikiliza kesi ya mteja wake ya madai ya talaka katika mahakama ya wilaya huko Luckenwalde, Brandenberg. 

Alisema mahakama ilitoa barua kwa mwanamke huyo kutii amri ya mahakama ya kuhudhuria kesi yake bila ya Hijabu vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa sheria ya Ujerumani ni kwamba wafanyakazi wa umma hawana ruhusa ya kuvaa mavazi yaanayoashiria dini lakini sheria hiyo haitumiki kwa watu wa kawaida .

Suala hilo limezua mjadala mkali kiasi cha msemaji wa mahakama hiyo kushindwa kutoa maoni yake licha ya kuulizwa na vyombo vya habari.

Sheria iliyopitishwa karibuni nchini Ujerumani ni ya kupinga vazi la Burqa na si Hijabu kwa wanawake wa kiislamu.

Ufaransa ndio nchi ya kwanza kwa ulaya kupiga marufu vazi la Burqa mwaka 2011 ikifuatiwa na nchi za Belgium na Bulgaria.