Polisi siku ya Ijumaa maeneo ya mitaa yaa zamani ya Jerusalem waliwazuia wanaume chini ya miaka 50 kutoshiriki ibada ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al aqsa.
Hata hivyo wanawake wenye umri zote walikubaliwa .
Hali ya ghasia na mvutano iliongezeka baada ya polisi wa Israel kuweka vizuizi vya chuma katika sehemu ya kuingia msikiti wa Haram al-Sharif .
Waislamu katika sehemu hiyo walilazimika kutekeleza ibada yao ya Ijumaa mitaani baada ya vizuizi hivyo vyenye chuma za kiddijitali kuwekwa .
Siku ya Alhamis Polisi waliwarushia waandamanaji wa kipalestinaa risasi za plastiki kwa madai kwamba walikuwa wamejihami kwa mawe .
Watu 37 wameripotiwa kujeruhiwa katika ghasia hizo .
Kiongozi mmojaa wa Israel alitangaza kwamba mamlaka imewapa polisi uhurru wa kuchukua hatua zozote ili kuhakikisha amani inaimarishwa katika maeneo matakatifu Jerusalem .