Saturday, 22 July 2017

APPLE WAZINDUA EMOJI YA MWANAMKE ALIYEVAA HIJABU

Kampuni ya Apple imezindua Emoji ya Hiijab katika siku ya kimataifa ya imoji. 

Siku ya kimataifa ya emoji hufanyika kila mwaka tarehe 17 julai. 

Emoji ni vibonzo vinavyotumika kuelezea katika kurasa za meseji kama WhatsApp nk kuelezea jambo badala ya maneno.
Kampuni hiyo ambyo hutengeza simu za iPhone, Mac na Ipad imefahamisha kuzindua Emoji mpya ya simu katika siku ya kimataifa ya Emoji .

Jumatatu kampuni hiyo imesema Emoji hiyo na zingine zaidi ya12 zitaanza kutumika kwa watumia wa toleo la la iOS 11.

Mbali na Emoji hiyo ya mwanamke anayeonekana kuvaa Hijabu pia yupo mwanaume anayeonekana amefuga ndevu.

Emoji hizo pia zitatumika katika mifumo mingine ya simu kama Android na Windows katika siku chache zijazo.