Monday, 26 June 2017

WAISLAMU KOTE DUNIANI WASHEHEREKEA SIKUKUU YA EID EL FITR

Leo waislamu duniani kote wamesheherekea sikukuu ya Eid el Fitr baada ya kumaliza ibada ya Funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waumini msikiti wa Kichangani Dar es salaam
Aidha pia baadhi ya nchi chache walisherehekea Sikukuu ya Eid el Fitr jana.

Baadhi ya nchi hizo ni Saudia Arabia, Misri, Pakistani, Afghanistan, Syria, Albania, Bangladeshi, Malaysia, Qatar, Uturuki na Ufaransa. Nchini Uingereza baadhi walisali Eid jana na wengine leo.


Waislamu wakisali Jijini Paris
Waliosali jana hufata kalenda ya Saudia na waliosali leo hufuata muandamo wa nchi ya Morocco.
Waislamu nchini Pakistan katika mji wa Peshawar
Nchini Tanzania Tanzania swala ya Eid el Fitr kitaifa imesaliwa Mkoa wa Kilimanjaro na mgeni rasmi katika baraza la Eid el Fitr anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.