Simu janja (Smartphone) kwa sasa ni sehemu muhimu katika maisha yetu. Ndani ya simu zetu kuna programu kwa ajili ya kila kitu.
Kutoka kuamka asubuhi, kuandaa mambo ya kikazi, kucheza michezo ya aina mbalimbali, ufuatiliaji wa uzito wako na kadhalika.
Pamoja na yote hayo pia kuna programu kwa ajili ya mambo ya kiroho, yaani mambo ya dini. Kwa mwezi huu wa Ramadhani kuna programu ambazo waislamu zinaweza kuwasaidia katika kuwaweka karibu na Mola wao ndani ya mwezi huu mtukufu.
Kuna programu maalumu na nyingi zilizoandliwa kwa ajili ya waislamu. Ni wakati mzuri wa kupakua kwa baadhi ya Progarmu hizo tutakazowawekea. Japo zipo nyingi lakini kwa leo tutawawekea sita tu.
1. Resala Ramadan
App hii itakusaidia kujua misingi ya kufunga katika mwezi wa Ramadhani. Pia utapata ujumbe tofauti tofauti kuhusu mwezi wa ramadhani kuhusu mambo ya halali na haramu na fadhila za kufunga. Aidha kuna maelezo jinsi Mtume ﷺ alivyokula daku na na kuftari. Maelezo yote yapo katika lugha za kiingereza , Kiarabu na Kiindonesia.
2. Salah 3D Pro Islam
App hii ni ya kujifuza namna ya kusali. Ni muhimu sana kwa watu wazima kujifunza namna ya kusali au kuwafundisha watoto namna ya kusali pia. Utajifunza na dua mbalimbali za ndani ya swala na namna ya kuchukua udhu pia. App hii ni kwa ajili yako.
3. Muslim Pro
App hii inatambuliwa na zaidi ya waislamu milioni 30 duniani kote. Kwenye App hii utapata kujua muda sahihi wa kuingia wakati wa Swala, kuweza kuweka Adhana katika simu yako. Pia utaweza kusikiliza wasomaji mbalimbali wa Qurani, kupata Kalenda ya kiislmau, Muelekeo wa Qibla, Ramani za migahawa ya Halal na misikiti popote ulipo.
4. Miftah Al-Quran
Ni App nzuri ya kujifunza jinsi ya kusoma Qurani kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka 4 mpaka 6. Aidha hata kwa watu wazima ni nzuri kujifunza kusoma na namna ya kuzitambua herufi za Qurani.
5. Ahbaabur Rasuul
Hii ni App iliyo katika lugha ya kiswahili. Itakuwezesha kupata habari mbalimbali za kiislamu popote duniani, makala na mawaidha. Itakusaidia kujua kinachoendelea katika ulimwengu wa kiislamu.
6. Islamic Greeting Cards
Ni App itakayokuwezesha kupata kwa urahisi kadi mbalimbali za kiislamu na kuweza kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki. Utapata kadi zenye aya mbalimbali, Hadithi za Mtume ﷺ na dua mbalimbali.