Nyota wa kiislamu wa timu ya Manchester City, Yaya Toure pamoja na wakala wake Dimitri Seluk wameahidi kuchangia Paundi milioni moja (Takribani Tshs Bilioni 2.8) ili kusaidia waathirika wa shambulizi la jumatatu iliyopita jiji la Manchester, Uingereza.
Toure na wakala wake waliahidi kila mmoja kutoa Paundi Elfu hamsini kwa wote walioathirika katika mkasa huo.
"Yaya ni kutoka Ivory Coast, mimi ni Urusi. Haijalishi. Leo ni nafasi kwa sisi watu wa soka kusaidia", alisema wakala wa Toure.
Aliongeza kusema kuwa wanataka kuwasaidia wahanga, familia za waliopoteza ndugu zao sambamba na wale waliopo hospitalini.
"Habari za kutisha Manchester, Mawazo na maombi yote kwa wale wote walioathirika", alitwiti Yaya toure katika ukurasa wake wa Twitter.
Takribani watu 22 walifariki na wengine 64 kujeruhiwa katika shambulizi hilo.