Saturday, 6 May 2017

MMISRI ATENGENEZA MSAHAFU WENYE MITA 700 KWA MKONO

Raia mmoja wa Misri anatumai kuweka historia baada ya kutumia muda wa miaka mitatu akitengeza kile kinachoonekana huenda ikawa Quran kubwa zaidi duniani.
Quran hiyo inayotengezwa na Saad Mohammed ambayo ameipamba, ina urefu wa mita 700 ikimaanisha kwamba inapofunguliwa ina urefu wa mita 381 sawa na jumba la Empire State.

Na kufikia sasa bwana Mohammed anayeishi katika mji wa Belqina kaskazini mwa Cairo amefadhili kila sentimita ya mradi wake.
Lakini ana matumaini makubwa. Anaamini kwamba kitabu hicho ni kirefu mno kuvunja rekodi za Guiness World Records ambapo hakuna rekodi iliowekwa ya Quran ndefu zaidi iliyoandikwa kwa mkono.
Lakini ili kufikia ndoto yake na kufanikiwa katika vitabu vya rekodi za Guiness anataka usaidizi wa gharama ya kuingia katika shindano hilo.

''Quran hii ina urefu wa mita 700 na kwa kweli hiyo ni karatasi kubwa sana'', aliiambia runinga ya Reuters.
''Nimejidhamini mwenyewe na mimi ni mtu wa mapato ya 
kawaida. Sina mali ama chochote kile''.