Thursday, 18 May 2017

MSIKITI WASHAMBULIWA NA KUUA WATU 20 NIGERIA

Watu 20 wamefariki katika shambulizi lililotekelezwa dhidi ya msikiti nchini Nigeria

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyanzo vya habari ni kwamba watu 20 wamefariki katika shambulizi lililotekelezwa dhidi ya msikiti.
Msemaji wa Polisi kwa jina lla Bala Elkana amesema kuwa huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka kufuatia shambulizi hilo.

Watu walioendesha shambulizi hilo bado hawajatambulika.

Mara kwa mara katika eneo hilo hutokea ghasia baina ya jamii ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo.

Jamii ya Fulani inatuhumiwa kuhusika na shambulizi hilo.

Watu  zaidi ya 400 wameripotiwa kufariki katika muda wa miaka miwili katika ghasia ambazo huzuka baina ya wafugaji na wakulima katika eneo hilo.