Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi kwa ajili ya vijana katika Ghuba ya Uajemi yatafanyika Muscat, Oman baadaye mwezi huu.
Kwa mujibu wa gazeti la al-Watan, mashindano hayo yatafanyika Februari 25 hadi Machi mbili.
Kamati ya maandalizi ya mashindano hayo imekutana hivi karibuni mjini Muscat kujadili nukta mbali mbali za mashindano hayo.
Katika kikao hicho, mkuu wa kamati maandalizi Muhammad bin Saed al Munawari na wanachama wengine walijadili njia za kuandaa mashindano bora.
Mashindano ya 28 ya Qur'ani Tukufu na Hadithi kwa ajili ya vijana katika Ghuba ya Uajemi hufanyika kila mwaka katika moja kati ya nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi
