Mcheza filamu nyota na mashuhuri wa Hollywood Mmarekani Morgan Freeman amesema adhana ni kati ya sauti bora zaidi duniani alizowahi kusikia.
Freeman ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati alipotembelea msikiti mjini New York na kuzungumza na Imamu na Muadhini akiwa katika mkakati wa kutegeneza filamu ijulikanayo kama ‘Kisa cha Mwenyezi Mungu’ inayogharamiwa na Shirika la National Geographic.
Katika kipindi hicho cha televisheni, Freeman anazungumza kuhusu historia ya dini ambapo anatembelea miji 20 katika nchi mbali mbali kufanya utafiti kuhusu Imani ya kidini.
Freeman aliuliza ni kigezo kipi ambacho hutumika kumchagua Muadhini. Aidha Freeman alijaribu kuadhini kwa kusema ‘Allahu Akbar’ na kisha akamuuliza Imamu iwapo sauti yake inafaa.
Imamu alimjibu kuwa anapaswa kufanya mazoezi ili aweze kuadhini kwa sauti inayotakiwa, Adhana ni wito wa Sala ambao hutulewa katika misikiti mara tano kwa siku kuwaita Waislamu watekeleza ibada ya sala.

