Wednesday, 10 August 2016

WATURUKI 60,000 WATARAJIWA KUTEKELEZA IBADA YA HIJJA MWAKA 2016

Mahajuji takriban 60,000 kutoka Uturuki mwaka 2016 watarajiwa kuanza kutekeleza ibada ya Hijja kwa mwaka 2016.
Kutoka mji wa Sakarya nchini Uturuki hujaji mwenye umri mdogo zaidi ni mtoto mchanga aliyezaliwa mnamo tarehe 27 mwezi Julai mwaka 2016 huku hujaji mzee kabisa mwenye umri wa miaka 100 aliyezaliwa mjini Malatya mnamo mwaka 1916 pia anatarajiwa kufanikisha ibada ya hajj mwaka 2016 .

Kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa idara ya masuala ya Hajj na Umrah zinaonyesha kuwa mwaka huu asilimia 43 ya mahujaji ni wanaume huku asilimia 57 ikiwa wanawake .

Ibada hiyo ya hajj itamalizika mnamo tarehe 17 mwezi Septemba mwaka huu. Mahujaji walitarajiwa kuanza rasmi safari yao ya kwenda kuhiji Makkah tarehe 4 mwezi Agosti.