Monday, 23 May 2016

MESUT OZIL ATUMIA SIKU ZA MAPUMZIKO KWENDA KUFANYA IBADA YA UMRA MAKKAH

Kiungo wa kati wa Ujerumani anayechezea kilabu ya Arsenal nchini Uingereza Mesut Özil, amezuru mji mtukufu wa Makkah nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya umrah.

Mesut Özil ambaye siku chache zilizopita alichaguliwa mchezaji bora wa Arsenal msimu huu, alisambaza picha alizopiga Makkah kwenye akaunti yake ya mtandao wa jamii wa Twitter na Instagram.

Maelfu ya mashabiki wa Mesut Özil wanaomfuatilia kwenye mitandao ya jamii walivutiwa mno na picha hizo alizosambaza mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid.

Mbele ya Al Qa'aba
Kutokana na ustadi wake aliouonyesha msimu huu na kilabu ya Arsenal, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameweza kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kwa ajili ya kucheza kwenye mashindano ya EURO 2016 nchini Ufaransa.

Kiungo wa Timu ya Arsenal Mesut Özil ametumia muda wake wa mapumziko baada ya kwisha kwa ligi za ulaya kwenda Makkah, Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya Ibada ya Umrah.
Özil aliweka picha yake akiwa mbele ya Al qa'aba kupitia akaunti yake ya Instagram.