Sunday, 1 May 2016

CHAMA KINACHOPINGA ADHANA, MINARA YA MSIKITI NCHINI UJERUMANI CHAPATA UPINZANI MKALI KWA WAANDAMANAJI

Polisi nchini Ujerumani wamewazuilia mamia ya waandamanaji wanaopinga chama cha mrengo wa kulia cha AFD chenye sera za kupiga vita Uislamu.
Waandamanaji
Chama hicho kinatarajiwa kuzinduliwa upya, na kutangaza wazi kuwa kinapinga dini ya kiislamu.
Chama hicho kinapanga kupiga marufuku vazi la kidini la burqa, minara ya misikiti na pia kupiga marufuku mwito wa waadhini yaani Adhana.

Zaidi ya maafisa 1000 wametumwa katika eneo la mkutano wa chama hicho katika mji wa Stuttgart kutoa ulinzi.
Kiongozi wa AFD
Polisi wametumia maji ya pilipili kuwatawanya waandamanaji waliobeba vijiti na vyuma, na kuchoma moto tairi kwenye kiingilio cha eneo la mkutano wa chama hicho, ili kuwazuia wanachama wake.