Doyin Okupe msemaji wa Ofisi ya Rais wa Nigeria amesema mgogoro ulioibuliwa na Boko Haram ni vita kamili. Amesema serikali ya Nigeria inakabiliana na adui mkubwa sana ambaye sasa amechukua mwelekeo wa kimataifa.
Katika tukio la hivi karibuni kabisa, siku ya Jumatatu wanamgambo wa Boko Haram waliishambulia shule moja ya bweni huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuuwa wanafunzi 59.
Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Maelfu ya watu wamepoteza maisha nchini Nigeria tokea kundi la Boko Haram lianzishe uasi mwaka 2009.
Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.
![]() |
| Boko Haram |
