Friday, 28 March 2014

PICHA: FILAMU YA NABII NUHU عليه السلام ILIYOPIGWA MARUFUKU NCHI ZA KIISLAMU

Filamu mpya ya Noah (Nabii Nuhu عليه السلام) ambayo imepigwa marufuku katika nchi za kiislamu inatarajiwa kuzinduliwa leo na kuoneshwa katika nchi mbalimbali duniani mwezi ujao mwaka huu.

Filamu hiyo imepigwa marufuku katika nchi nyingi za kiislamu kutokana na filamu hiyo kuwa kinyume na maadili ya kiislamu. Nuhu  عليه السلام ni mmoja wa manabii wa kiislamu.

kutangaza kuipiga marufuku filamu mpya iliyotengenezwa Hollywood, Marekani inayoitwa Noah (Nuhu) ambayo inaelezea maisha ya Nabii Nuhu  عليه السلام kwa msingi wa Kitabu cha Biblia.

Nchi za Qatar, Indonesia, Bahrain na Falme za Kiarabu tayari zimeipiga marufuku filamu hiyo. Aidha wanazuoni wa Misri pia wametoa wito ipigwe marufuku nchini Misri.

Angalia picha za matukio mbalimbali katika filamu hiyo.